Warumi 4 – Ibrahimu na Daudi wanadhihirisha haki kando na Matendo
A. Ibrahimu anatangazwa kuwa mwadilifu kupitia imani.
1. (1–3) Ibrahimu hakuhesabiwa haki kwa matendo, bali alihesabiwa haki kwa imani.
Tuseme nini basi; kwamba Ibrahimu,amekuwa baba yetu, kwa jinsi ya mwili? ikiwa Ibrahimu alihesabiwa haki kwa matendo, analo la kujivunia, lakini si mbele za Mungu. Maandiko yanasemaje? “Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa haki.”
a. Tuseme nini basi: Katika kujenga juu ya wazo lililoanza katika Warumi 3:31, Paulo anauliza swali, “Je! wazo la kuhesabiwa haki kwa njia ya imani pasipo matendo ya sheria, linafanya kile ambacho Mungu alitenda katika agano la kale kuwa yasiyo na maana?
b. Ni nini basi tutasema Ibrahimu baba yetu amepata? Kwa kujibu swali hilo, Paulo anamtazama Ibrahimu, ambaye alikuwa mtu aliyeheshimiwa sana miongoni mwa Wayahudi wa siku zake – hata mkuu kuliko George Washington wa Marekani.
c. Kwa maana ikiwa Ibrahimu alihesabiwa haki kwa matendo, analo la kujisifu: Ikiwa mtu yeyote angeweza kuhesabiwa haki kwa matendo, angekuwa na kitu cha kujisifu. Hata hivyo majivuno ya namna hiyo sio kitu mbele za Mungu (lakini si mbele za Mungu).
i. Kujisifu huku si kitu mbele za Mungu kwa sababu hata kama matendo yangeweza kumfanya mtu kuwa na haki, kwa namna fulani bado angepungukiwa na utukufu wa Mungu (Warumi 3:23).
ii. Kujisifu huku si kitu kwa sababu mbele za Mungu, kila kujifanya kunaondolewa na ni dhahiri hakuna mtu anayeweza kuhesabiwa haki kwa matendo.
d. Kwa maana Maandiko yanasemaje? Agano la Kale halisemi Ibrahimu alitangazwa kuwa mwenye haki kwa sababu ya matendo yake. Badala yake, Mwanzo 15:6 inasema kwamba Ibrahimu alimwamini Mungu na ikahesabiwa kwake kuwa haki.
i. Paulo anaweka wazi: Haki ya Ibrahimu haikutokana na kutenda matendo mema, bali kwa imani katika Mungu. Ilikuwa ni haki ipatikanayo kwa njia ya imani.
ii. Kwa ujumla, walimu wa Kiyahudi wa siku za Paulo waliamini kwamba Ibrahimu alihesabiwa haki kwa matendo yake, kwa kushika sheria. Vifungu vya kale kutoka kwa marabi vinasema: “Tunaona kwamba Ibrahimu baba yetu alikuwa ametunza Sheria yote kabla haijatolewa” na “Abrahamu alikuwa mkamilifu katika matendo yake yote mbele za Bwana.” Marabi walibishana kwamba Ibrahimu aliishika torati kikamilifu kabla haijatolewa, akiitunza kwa kudhaniwa au kutazamia.
iii. Mtume Paulo hasemi Ibrahamu alifanywa kuwa mwadilifu katika matendo yake yote, lakini Mungu alimhesabia Ibrahamu mwadilifu. Kuhesabiwa haki kwetu si Mungu kutufanya waadilifu kikamilifu, bali anatuhesabu kuwa wenye haki kabisa. Baada ya kuhesabiwa kuwa wenye haki, ndipo Mungu anaanza kutufanya kuwa wenye waadilifu kweli, na kufikia kilele chake katika ufufuo wetu.
iv. Kuhesabiwa ni logizomai. Ilitumika katika hati za kale za kidunia; ‘weka kwenye akaunti ya mtu, mapato yangu na yawekwe kwenye akiba katika ghala, Sasa natoa maagizo kwa ujumla kuhusu malipo yote yanayofanywa au kutumwa kwa serikali.’ Hivyo, Mungu akaweka katika hesabu ya Ibrahimu, iliyowekwa kwa ajili yake, iliyohesabiwa kwake, haki… Ibrahimu alikuwa na haki kama vile mtu angekuwa na kiasi cha fedha kilichowekwa katika akaunti yake katika benki. (Wuest)
v. Mwanzo 15:6 haituelezi jinsi watu wengine walivyomhesabia Ibrahamu. Badala yake, inatuambia jinsi Mungu alivyomhesabu. “Musa [katika Mwanzo] hatuelezi, kwa hakika, vile watu walifikiri juu yake [Ibrahamu], bali jinsi alivyohesabiwa mbele ya mahakama ya Mungu.” (Calvin)
vi. Kumbuka haki pia ni zaidi ya kutokuwepo kwa uovu na hatia. Ni wema, ikimaanisha kwamba Mungu hatutangazi tu kuwa hatuna hatia, bali ni wenye haki.
2. (4-5) Tofauti iliyowekwa kati ya neema na matendo.
Basi kwa mtu afanyaye kazi, mshahara hauhesabiwi kuwa ni neema, bali ni deni. Lakini kwake yeye asiyefanya kazi, bali anamwamini yeye ambaye anayemhesabia haki asiye mcha Mungu, imani yake mtu huyo inahesabiwa kuwa haki.
a. Basi kwa mtu afanyaye kazi, mshahara wake hauhesabiwi kuwa ni neema: Wazo la neema ni kinyume cha kanuni ya matendo; neema inahusiana na kupokea karama iliyotolewa bure na Mungu, kazi zinahusiana na kupata stahili yetu mbele za Mungu.
i. Wuest juu ya ‘charis’, neno la kale la Kigiriki lililotafsiriwa neema: “Iliashiria katika waandishi wa kitambo upendeleo unaofanywa kutokana na ukarimu au hiari wa moyoni bila kutarajia wala kupokea. Bila shaka, upendeleo huu siku zote ulifanywa kwa rafiki wa mtu, sio kwa adui… Lakini hisani inapoingia katika Agano Jipya, inachukua hatua ya mbele isiyo na kikomo, neema ambayo Mungu alifanya pale Kalvari ilikuwa kwa wale waliomchukia.”
b. Haihesabiwi kama neema lakini kama deni: Mfumo wa kazi unatafuta kumweka Mungu katika hali ya kuwa na deni kwetu, na kumfanya Mungu atuwie kibali chake kwa sababu ya tabia yetu nzuri. Katika kuwaza-matendo, Mungu ni mdeni wetu wa wokovu au baraka kwa sababu ya matendo yetu mema.
i. Mungu asifu uvivu hapa.Upinzani sio tu kati ya mfanyakazi na asiye wa kazi lakini kati ya mfanyakazi na mtu ambaye hafanyi kazi lakini anaamini. (Murray)
c. Lakini kwa mtu asiyefanya kazi, bali anamwamini anayewahesabia haki wasiomcha Mungu, imani yake inahesabiwa kuwa haki: Haki haiwezi kamwe kuhesabiwa kwake mtu anayemkaribia Mungu kwa kanuni ya matendo. Badala yake inatolewa kwa yule amwaminiye huwahesabia haki wasiomcha Mungu.
d. Yeye anayewahesabia haki wasio mcha Mungu: Huyu ndiye Mungu humhesabia haki – muovu. Tunaweza kutarajia Mungu angemhesabia haki mtu mcha Mungu lakini kwa yale Yesu alifanya msalabani, Mungu anaweza kuwahesabia haki waouvu.
i. Sio kwamba Mungu anafurahishwa na hali yetu ya kutomcha Mungu. Hatuhesabiwi haki kwa sababu ya uasi wetu, bali pasipo kujali uasi wetu.
ii. Morris akimnukuu Denney: “Kifungu cha maneno yanayo kinzana Yeye anayewahesabia haki wasiomcha Mungu, hakipendekezi kuhesabiwa haki ni hekaya, iwe ya kisheria au ya aina nyingine yoyote, bali kwamba ni muujiza.”
e. Imani inahesabiwa kuwa haki: kama vile Ibrahamu, imani yetu inahesabiwa kuwa haki. Huu haukuwa mpango maalum kwa Ibrahamu pekee. Tunaweza kuingia katika uhusiano huu na Mungu pia.
i. Kwa hili tunaelewa hakuna njia mbili za wokovu – kuokolewa kwa matendo kupitia kushika sheria katika Agano la Kale na kuokolewa kwa neema kupitia imani katika Agano Jipya. Kila mtu ambaye amewahi kuokolewa – Agano la Kale au Jipya – anaokolewa kwa neema kupitia imani, kupitia uhusiano wao wa upendo wa kuaminiana na Mungu. Kwa sababu ya Agano Jipya tuna faida za wokovu ambazo watakatifu wa Agano la Kale hawakuwa nazo lakini hatuna namna tofauti ya wokovu.
3. (6–8) Daudi na baraka ya kuhesabiwa haki kwa imani.
Kama vile Daudi pia anavyoeleza heri ya mtu ambaye Mungu humhesabia kuwa haki pasipo matendo:
“Heri waliosamehewa matendo yao maovu,
na ambao dhambi zao zimefunikwa;
Heri mtu yule ambaye BWANA hatamhesabia dhambi.”
a. Kama vile Daudi pia anavyoeleza: Mfalme Daudi wa Agano la Kale alijua jinsi ilivyokuwa kuwa mtenda dhambi mwenye hatia. Alijua uzito wa dhambi na jinsi ilivyo vizuri kusamehewa kabisa. Alijua baraka ya mtu ambaye Mungu humhesabia haki bila matendo. Ikiwa Daudi alihukumiwa kwa matendo peke yake, Mungu mwenye haki lazima amhukumu; walakini alijua kwa uzoefu heri wale ambao matendo yao maovu yamesamehewa.
i. “Hakuna mwenye dhambi, na kujaribu kwa bidii sana, anaweza kubeba dhambi zake mwenyewe na kurudi akiwa amesafishwa na bila hatia. Hakuna kiasi cha fedha, bila sayansi, bila ujuzi wa uvumbuzi, bila majeshi ya mamilioni, wala nguvu nyingine yoyote ya kidunia inayoweza kumuondolea mwenye dhambi, dhambi moja ndogo na hatia yake. Mara tu inapofanywa, kila dhambi na hatia yake hushikamana na mdhambi kama vile kivuli chake mwenyewe, ikishikamana na umilele wote isipokuwa Mungu ataziondoa.” (Lenski)
b. Ambaye Mungu humhesabia haki pasipo matendo… heri Bwana hatamhesabia dhambi: Daudi anakubaliana na Ibrahimu kuhusu wazo la kuhesabiwa haki, wema unaotolewa, ambao haukutendewa.
i. “Wapinzani wetu wafuasi wa papa wanapinga kuhesabiwa kwa haki ya Kristo kwetu; wanalichukia neno hilo… hata ingawa bado mtume ametumia neno hili mara kumi katika sura hii.” (Poole)
c. Mbarikiwa ni yule: Katika Zaburi iliyonukuliwa (Zaburi 32:1–2), Daudi anazungumza juu ya baraka, si ya yule anayehesabiwa haki kupitia matendo, bali juu ya yule anayetakaswa kwa uwakilishi. Hii inazingatia kile Mungu anaweka juu yetu (haki ya Yesu), sio wa kile tunachofanya kwa ajili ya Mungu.
4. (9–12) Ibrahamu alihesabiwa kuwa mwadilifu kabla ya kutahiriwa; kwa hivyo hakuhesabiwa kuwa mwenye haki kwa sababu ya kutahiriwa.
Je Baraka hii huwapata waliotahiriwa pekee, au wale pia wasiotahiriwa? Kwa maana twasema imani ilihesabiwa kwa Ibrahamu kuwa haki. Ilihesabiwaje basi? Akiwa ametahiriwa au hajatahiriwa? Si wakati ametahiriwa, lakini wakati bado hajatahiriwa. Naye alipokea ishara ya kutahiriwa, muhuri ya haki ya imani aliyokuwa nayo kabla hajatahiriwa, ili awe baba yao wote waaminio, ingawa hawajatahiriwa, ili wao pia wahesabiwe haki; baba wa tohara kwa wale sio waliotahiriwa tu, bali pia wanaoenenda katika hatua za imani ambazo baba yetu Ibrahimu alikuwa nazo kabla hajatahiriwa.
a. Je, basi, baraka hii huwapata wale waliotahiriwa tu, au pia kwa wale wasiotahiriwa? Ikiwa tunahesabiwa kuwa waadilifu na Mungu kwa sababu ya imani, si kwa sababu ya kutahiriwa (au desturi nyingine yoyote), basi baraka inayotajwa katika Warumi 4:7 inaweza kutolewa kwa Wamataifa wasiotahiriwa kwa imani.
b. Ilihesabiwaje? Akiwa ametahiriwa au hajatahiriwa? Ibrahimu alihesabiwa kuwa mwenye haki katika Mwanzo 15:6. Hakupokea agano la tohara hadi Mwanzo 17, ilikuwa angalau miaka 14 baadaye. Kwa hiyo haki yake haikuwa kwa tohara, bali kwa imani.
c. Imani aliyokuwa nayo kabla ya kutahiriwa: Hakika, Ibrahamu, baba wa wale wote wanaoamini, alitangazwa kuwa mwadilifu kama hajatahiriwa! Kwa hiyo, basi, mtu angewezaje kusema (kama wengine walivyosema katika siku za Paulo) kwamba ni lazima watu wa mataifa mengine watahiriwe kabla Mungu hajawatangaza kuwa wenye haki?
i. Kwa Wayahudi wa siku za Paulo, umuhimu wa tohara ulikuwa zaidi ya kijamii. Ilikuwa ni mahali pa kuingilia maisha yaliyoishi chini ya Sheria ya Musa: Nami namshuhudia tena kila mtu ametahiriwa kuwa ana deni la kuishika torati yote (Wagalatia 5:3).
d. Ili apate kuwa baba yao wote waaminio, ijapokuwa hawajatahiriwa… wanaoenenda pia katika hatua za imani aliyokuwa nayo baba yetu Ibrahimu alipokuwa bado hajatahiriwa: Wayahudi wa siku za Paulo walifikiri kutahiriwa kulimaanisha kuwa wao ndio walikuwa wazao wa kweli wa Ibrahimu. Paulo anasisitiza ili Ibrahimu awe baba yenu, ni lazima mtembee katika hatua za imani ambazo Ibrahamu alifuata.
i. “Baba yetu Ibrahimu” ni kifungo cha maneno muhimu, ambacho Wayahudi wa kale walilinda kwa wivu. Hawakumruhusu mtu wa Mataifa aliyetahiriwa, aliyebadilishwa katika Uyahudi amwite Ibrahimu “baba yetu” hata katika sinagogi. Mwongofu asiye Myahudi ilimbidi kumwita Ibrahimu “baba yenu” na ni Wayahudi wa asili ya kuzaliwa pekee walioweza kumwita Ibrahamu “baba yetu.” Paulo Anatupilia mbali tofauti hiyo, na kusema kwa imani, wote wanaweza kusema, “Baba yetu Ibrahimu”.
ii. Lazima iliwashtua wasomaji Wayahudi wa barua hii kuona kwamba Paulo alimwita Ibrahamu baba wa watu wasiotahiriwa! Imani, si tohara, ndicho kiungo muhimu kwa Ibrahimu. Ni muhimu sana kuwa na imani ya Ibrahimu (na haki iliyohesabiwa kwake kwa ajili ya imani) kuliko kutahiriwa kwa Ibrahimu.
iii. William Barclay aeleza walimu Wayahudi wa siku za Paulo walikuwa na msemo huu: “Yale yaliyoandikwa juu ya Ibrahamu yameandikwa pia kuhusu watoto wake,” ikimaanisha kwamba ahadi alizopewa Ibrahamu zilienea kwa kizazi chake. Paulo alikubaliana kwa moyo wote na kanuni hii, na kupanua kanuni ya kuhesabiwa haki kwa imani kwa wazao wote wa kiroho wa Ibrahimu, wale wanaoamini, ambao pia huenenda katika hatua za imani ya Ibrahimu.
5. (13–15) Ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu ilijengwa juu ya kanuni ya imani, si sheria au matendo.
Kwa maana ahadi ya atakuwa mrithi wa ulimwengu haikuwa kwa Ibrahimu wala kwa uzao wake kwa njia ya sheria, bali kwa njia ya haki kwa imani. Ikiwa wale wa sheria ndio warithi, imani imekuwa ubatili na ahadi imebatilika, kwa sababu sheria huleta ghadhabu, maana pasipokuwa na sheria hauna kosa.
a. Kwa maana ahadi ya kuwa mrithi wa ulimwengu haikuwa kwa Ibrahimu au kwa uzao wake kwa njia ya sheria: Shughuli zote za Mungu na Ibrahamu, Isaka, na Yakobo zilifanyika kabla ya kutolewa kwa Sheria ya Musa, hatuwezi kusema zilitokana na sheria. Badala yake, zinatokana na uamuzi wa Mungu wa haki kwa Ibrahimu kwa njia ya imani.
i. “Imani ndiyo msingi wa baraka za Mungu. Ibrahimu alikuwa mtu aliyebarikiwa, kwa kweli, lakini akawa mrithi wa ulimwengu kwa kanuni nyingine kabisa – imani rahisi. (Newelli)
b. Kwa ahadi… kwa njia ya haki ya imani: Sheria haiwezi kutuleta katika baraka za ahadi za Mungu. Si kwa sababu sheria ni mbaya, bali ni kwa sababu hatuwezi kuitunza.
c. Kwa sababu sheria huleta ghadhabu: Kutoweza kushika sheria (makosa yetu) ina maana kwamba inakuwa hasa chombo cha kuleta ghadhabu ya Mungu kwetu, hasa ikiwa tunaiona kama kanuni ambayo tunahesabiwa haki na kuhusiana na Mungu.
d. Pale ambapo hakuna sheria hakuna makosa: Je, Paulo anawezaje kusema hili? Kwa sababu Ukiukaji ni neno sahihi kwa kuvuka mstari, na hii ni wazi kwa kuvunja amri iliyolainishwa wazi (Morris).Mahali hakuna mstari, hakuna makosa halisi.
i. Kuna dhambi ambayo sio “kuvuka mstari” Sheria ya Musa. Mzizi wa dhambi hauko katika kuvunja sheria, bali katika kuvunja imani na Mungu; kwa kukataa kusudi lake la upendo na kujali katika kila amri anayotoa. Kabla Adamu hajatenda dhambi alivunja uaminifu kwa Mungu – kwa hiyo mpango wa Mungu wa ukombozi umejikita katika uhusiano wa upendo wa kutumainia – imani – badala ya kushika sheria. Tunapoweka uhusiano wetu na Mungu kwenye kushika sheria badala ya upendo wa kutumainia, tunaenda kinyume na mpango Wake wote.
B. Kufuata mfano wa Ibrahimu.
1. (16) Kuhesabiwa haki kulingana na neema, kwa njia ya imani.
Ni kwa imani,ili iwe kwa neema, ili ahadi iwe imara kwa wazao wote, si kwa wale wa sheria tu, bali pia kwa wale walio wa imani ya Ibrahimu, aliye baba yetu sisi sote
a. Ni kwa imani kwamba inaweza kuwa kulingana na neema: Imani inahusiana na neema kwa njia sawa jinsi matendo yanayohusiana na sheria. Neema na sheria ni kanuni, na imani na matendo ni njia ambayo kwayo tunafuata kanuni hizo kwa ajili ya uhusiano wetu na Mungu.
i. Kuzungumza kiujuzi, hatuokolewi kwa imani. Tunaokolewa kwa neema ya Mungu, na neema inamilikiwa kwa imani.
b. Ni kwa imani: Wokovu ni wa imani na sio kitu kingine. Tunaweza tu kupokea wokovu kwa kanuni ya neema kupitia imani. Neema haiwezi kupatikana kupitia kazi, iwe ni kazi zilizopita, kazi za sasa, au kazi zilizoahidiwa. Hii ni kwa ufafanuzi neema hutolewa bila kujali chochote kwa yule anayeipokea.
i. Neema na imani zinaambatana, na zitavutwa pamoja katika gari moja, lakini neema na sifa ni kinyume na huvuta njia tofauti, kwa hivyo Mungu hakuchagua kuzifunga pamoja. (Spurgeon)
c. Ili ahadi iwe ya hakika kwa wazao wote: Ahadi inaweza kuwa ya hakika ikiwa ni kulingana na neema. Ikiwa sheria ndiyo msingi wa wokovu wetu, basi wokovu wetu unategemea utendaji wetu katika kushika sheria – na hakuna mtu anayeweza kutunza sheria vizuri vya kutosha kuokolewa kwayo. Ahadi ya sheria ya wokovu haiwezi kamwe kuwa na uhakika.
i. Ikiwa ahadi “ingekuwa ya sheria, isingekuwa ya hakika na ikose uyakini, kwa sababu ya udhaifu wa mwanadamu, asiye weza kuitimiza.” (Poole)
d. Lakini pia kwa wale walio wa imani ya Ibrahimu, ambaye ni baba yetu sote: Ikiwa uhusiano wetu na Mungu ni wa neema (sio tohara au kushika sheria), basi uhusiano huo ni kwa wale ni wa imani ya Ibrahim, hata kama wao si wa ukoo wake.
i. Mmataifa angeweza kusema, “Mimi si Myahudi, mimi si wa sheria; bali mimi ni wa imani ya Ibrahimu,” naye angeokolewa sawa na vile mwumini wa Kiyahudi katika Yesu angeokolewa.
e. Baba yetu sote: Utimilifu wa ahadi katika Mwanzo 17:4-5 haupatikani katika uzao wa Ibrahimu kupitia Isaka, lakini katika jukumu yake kama baba yetu sisi sote tunaoamini – na waumini hao wanatoka katika kila taifa. chini ya mbingu.
2. (17–18) Uweza wa utoaji uzima wa Mungu ambaye Ibrahimu alimwamini.
(kama ilivyoandikwa, Nimekufanya wewe kuwa baba wa mataifa mengi) mbele zake yeye aliyemwamini; Mungu anaye fufua wafu na kuviita visivyokuwepo vilikuwako; ambaye kinyume na tumaini aliamini kwa kutumaini, hata akawa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.
a. Kwa hiyo akawa baba wa mataifa mengi: Kama vile iliwagharimu kazi isiyo ya kawaida ya kutoa uhai ili kumfanya Ibrahimu baba wa kimwili wa mataifa mengi, pia ilihitaji kazi isiyo ya kawaida yenye kutoa uhai ili kumfanya baba wa kiroho wa mataifa mengi.
b. Ambaye hufufua wafu na kuviita visivyokuwepo vilikuwako: Matendo haya ya Mwenyezi Mungu yanadhihirisha uwezo wake wa kuhesabu vitu visivyokuwa (kama vile haki yetu) kwamba viko (kama kutuhesabia haki).
i. Ikiwa Mungu angeweza kuliita tumbo la uzazi la Sara lililokufa, anaweza kuwaita wale waliokufa kwa sababu ya makosa na dhambi (Waefeso 2:1) kwenye uzima mpya katika Yesu.
ii. “Ninafarijiwa sana Mungu anapozungumza kunihusu kama mwenye haki,aliyethibitishwa, mwenye utukufu, mtakatifu, msafi na aliyetakaswa. Mungu anaweza kuzungumza juu ya mambo hayo kabla hayajatokea, kwa sababu anajua yatakuwapo.” (Smith)
c. Kinyume na tumaini, kwa matumaini waliamini: Nguvu hii ya utoaji uzima ilitimizwa kwa Ibrahimu kama alivyoamini. Nguvu zilionekana kwa kimwili na kiroho.
i. Mfano wa Ibrahamu hutusaidia pia kuelewa uhalisi wa imani. Mimba ya mwana wa Ibrahimu Isaka ilikuwa muujiza, lakini haikuwa mimba safi. Imani ya Ibrahimu haikumaanisha kwamba hakufanya lolote aligoja tu Mungu aumbe mtoto katika tumbo la Sara. Ibrahamu na Sara walikuwa na uhusiano wa ndoa na walimtumaini Mungu kwa matokeo ya kimuujiza. Hii inatuonyesha imani haimaanishi kutofanya lolote, bali kufanya kila kitu kwa imani na kumtegemea Mungu.
ii. “Waumini wote waaminifu, kama Ibrahimu, wanatii. Kutii ni imani katika matendo. Unapaswa kuenenda katika hatua za imani ya baba Ibrahimu. Imani yake haikukaa tuli, ilichukua hatua; na lazima uchukue hatua hizi pia kwa kumtii Mungu kwa sababu unamwamini. Ile imani isiyo na matendo ni imani ambayo imekufa, wala haitamhesabia mtu haki.(Spurgeon)
iii. Hisia husahihisha mawazo, fikra husahihisha akili, lakini imani husahihisha zote mbili. Haitakuwa, asema akili; haiwezi kuwa, inasema fikra; inaweza na itakuwa, imani yasema, kwa maana ninayo ahadi kwa hilo.” (Trapp)
3. (19–22) Tabia ya imani ya Ibrahimu.
Na hakuwa dhaifu katika imani, hakuhesabu mwili wake uliokuwa umekwisha kufa (tangu alikuwa na umri wa miaka karibia mia moja), na hali ya kufa kwa tumbo la Sara. Hakusitasita katika ile ahadi ya Mungu kwa kutoamini, bali alitiwa nguvu katika imani, akimtukuza Mungu, akiwa na hakika kabisa yale aliyoahidi angeweza pia kufanya. Na kwa hiyo “ilihesabiwa kwake kuwa haki.”
a. Kutokuwa dhaifu katika imani: Imani ya Ibrahimu ilikuwa na nguvu lakini pia ilitiwa nguvu. Aliimarishwa katika imani.
i. Wazo linaonekana kuwa Ibrahimu aliimarishwa katika imani yake; lakini Paulo pia angeweza kumaanisha Ibrahimu aliimarishwa na imani yake – hakika wote wawili walikuwa kweli.
ii. Jinsi tunavyohitaji kuimarishwa katika imani! ’Ndugu mpendwa, imani ndogo itakuokoa ikiwa ni imani ya kweli, lakini kuna sababu nyingi kwa nini unapaswa kutafuta ongezeko hilo.’ (Spurgeon)
iii. Spurgeon alijua wahudumu na wahubiri walihitaji hasa kuimarishwa katika imani. Wakati fulani alishiriki mapambano yake mwenyewe katika eneo hili kutoka kwenye mimbari, lakini alitaka kuweka wazi mapambano yake katika imani hayapaswi kamwe kuchezewa: “Wasikilizaji wapendwa, mnapompata yeyote miongoni mwetu ambaye ni walimu akiwa na mashaka na woga, msihurumie, lakini mtukaneni. Hatuna haki ya kuwa katika Jumba la Mashaka. Omba usitutembelee huko. Tufuate kadiri tunavyomfuata Kristo, lakini ikiwa tunaingia katika Unyogovu wa kutisha wa Kukata tamaa, njoo utuvute kwa nywele za vichwa vyetu ikiwa ni lazima, lakini wewe mwenyewe usianguke ndani yake. (Spurgeon)
iv. “Sidhani kama tutakuwa na mazungumzo mengi isipokuwa tukitazamia Mungu kubariki neno, na kuhisi hakika atafanya hivyo. Hatupaswi kushangaa na kustaajabu ikiwa tunasikia juu ya dazeni moja au mbili za kuokoka, lakini acha mshangao uwe maelfu hawaokoki wanaposikia ukweli huo wa kimungu, na tunapomwomba Roho Mtakatifu ahudhurie kwa nguvu za kiungu. Mungu atatubariki kwa kadiri ya imani yetu. Ni kanuni ya ufalme wake – ‘Kwa mujibu wa imani yako na iwe hivyo kwako.’ Ee Mungu, wape wahudumu wako imani zaidi! Hebu tukuamini kabisa!” (Spurgeon)
b. Yeye hakukizingatia mwili wake uliokuwa umekufa: Ibrahimu, katika imani, hakutazamia hali (mwili wake mwenyewe na kufa kwa tumbo la uzazi la Sara) bali aliitazama ahadi ya Mungu.
i. Katika Warumi 4:19, kuna kutokuwa na hakika kwa maandishi tunapaswa kusoma aliona mwili wake bora kama mfu au ikiwa tunapaswa kusoma hakuzingatia mwili wake mwenyewe. Aidha inawezekana, ingawa ya pili inaonekana kuwa chaguo bora.
c. Yeye hakusitasita katika ahadi ya Mungu kwa kutoamini: Imani yake haikutikisika; nayo ikamtukuza Mungu. Ingawa ilikuwa changamoto kubwa, Ibrahimu alibaki imara katika imani.
i. “Wakati hakuna mashindano, ni kweli, hakuna mtu, kama nilivyosema, anayekataa Mungu anaweza mambo yote; lakini mara tu jambo lolote linapotokea kuzuia njia ya ahadi ya Mungu, tunatupa nguvu ya Mungu kutoka katika ukuu wake.” (Calvin)
d. Akiwa amesadiki kabisa kile alichoahidi pia alikuwa na uwezo wa kufanya: Imani ya Ibrahimu ilikuja kwa sababu alikuwa ameamini kwa hakika Mungu ana uwezo wa kufanya yale aliyoahidi.
i. Mungu wako ni mdogo sana? Mungu wa Ibrahimu aliweza kufanya yale aliyoahidi, na Ibrahimu alikuwa na uhakika juu yalo.
ii. Watu wengine hawaji kwa Yesu au hawaendi mbali zaidi Naye kwa sababu hawajaamini kwa hakika kwamba kile alichoahidi pia alikuwa na uwezo wa kufanya. Wanafikiri, Ni sawa kwa wengine lakini haitafanya kazi kwangu, Mawazo haya ni uvamishi wa kishetani dhidi ya imani, na lazima yakataliwe.
e. Uwezo wa kutenda: Aina hii ya imani huona kazi ya Mungu ikifanywa. Inachunguza kazi ya Mungu iliyofanywa mara moja (Isaka alizaliwa katika utimilifu wa ahadi) na katika umilele (ilihesabiwa kwake kuwa haki).
4. (23–25) Kuhesabiwa haki kwa Ibrahimu na sisi wenyewe.
Basi haikuandikwa kwa ajili yake peke yake kwamba ilihesabiwa kwake, pia kwa ajili yetu. Itahesabiwa kwetu sisi tunaomwamini yeye aliyemfufua Bwana wetu Yesu kutoka kwa wafu, ambaye alitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa kwa kuhesabiwa haki kwetu.
a. Haikuandikwa kwa ajili yake peke yake: Haikuwa tu kwa faida ya Ibrahamu Mungu alimtangaza kuwa mwadilifu kwa njia ya imani; yeye ni mfano ambao tunaalikwa kufuata – ni kwa ajili yetu pia. Ujasiri wa Paulo ni wa utukufu: Itahesabiwa kwetu sisi tunaoamini; hii haikuwa kwa ajili ya Ibrahimu pekee, bali kwa ajili yetu pia.
b. Wanaomwamini Yeye aliyemfufua Yesu: Tunapozungumza juu ya imani na imani inayookoa katika Yesu, ni muhimu kusisitiza kuwa tunamaanisha kuamini kazi yake msalabani (iliyotolewa kwa sababu ya makosa yetu) na ushindi juu ya dhambi na kifo (iliyoinuliwa kwa sababu ya kuhesabiwa haki kwetu) ndiyo inayotuokoa. Kuna imani nyingi za uwongo ambazo haziwezi kamwe kuokoa, na imani tu katika yale ambayo Yesu alitimiza msalabani na kupitia kaburi wazi inaweza kutuokoa.
∙ Imani katika matukio ya kihistoria maisha ya Yesu haitaokoa.
∙ Imani katika uzuri wa maisha ya Yesu hautaokoa.
∙ Imani katika usahihi au wema wa mafundisho ya Yesu haitaokoa.
∙ Imani katika uungu wa Yesu na katika Ukuu wake haitaokoa.
∙ Ni Imani tu katika yale ambayo Yesu alitenda kwa ajili yetu msalabani itaokoa.
c. Kufufuliwa kwa sababu ya kuhesabiwa haki kwetu: Ufufuo una nafasi muhimu katika ukombozi wetu kwa sababu unaonyesha kuridhika kamili kwa Mungu Baba na kazi ya Mwanawe msalabani.Inathibitisha kile Yesu alichofanya msalabani kwa hakika ilikuwa ni dhabihu kamilifu iliyotolewa na Yule ambaye alibaki mkamilifu, ingawa alikuwa amebeba dhambi ya ulimwengu.
i. Kutolewa kwa sababu ya makosa yetu: Neno la kale la Kigiriki lililotafsiriwa kutolewa (paradidomi) lilitumiwa kuwatupa watu gerezani au kuwapeleka mbele ya haki. “Hapa linazungumza juu ya tendo la hukumu ya Mungu Baba kumtoa Mungu Mwana kwenye haki ambayo ilihitaji malipo ya adhabu ya dhambi ya wanadamu.” (Wuest)
ii. “Siku zote ufufuo wa Yesu hujumuisha kifo chake cha dhabihu lakini unaonyesha utoshelevu wa kifo chake. kama mauti yangemshika, hangefaulu; kwa kuwa alifufuka katika wafu, dhabihu yake ilitosha, Mungu aliweka muhuri juu yake kwa kumfufua.” (Lenski)
iii. “Kristo alitenda kwa heshima kuhesabiwa haki na wokovu wetu kwa kifo na mateso yake, lakini ufanisi na ukamilifu wake kuhusiana nasi hutokana na ufufuo wake… Mstari huu mmoja ni uunganisho wa injili yote.” (Pooli)
iv. Katika sura hii, Paulo alionyesha wazi Agano la Kale halipingi injili ya wokovu kwa neema kupitia imani. Badala yake injili ni utimilifu wa Agano la Kale, na Ibrahimu – kuhesabiwa haki kwa imani – ndiye kielelezo chetu.
© 2024 The Enduring Word Bible Commentary by David Guzik – ewm@enduringword.com