Warumi 3 – Kuhesabiwa bure kwa Neema yake
A. Haki ya hukumu za Mungu.
1. (1–2) Faida ya Wayahudi.
Myahudi ana faida gani basi, au kutahiriwa kuna faida gani? Mengi kwa kila njia! Hasa kwa sababu yamekabidhiwa maneno ya Mungu.
a. Myahudi ana faida gani basi: Paulo ameeleza kwa makini katika Warumi 2 kuwa na sheria au kutahiriwa hakutamwokoa Myahudi. Ikiwa hivyo, basi kuna faida gani ya kuwa “taifa teule la Mungu”?
i. Baada ya yote, ikiwa hakuna upendeleo kwa Mungu (Warumi 2:11), kuna faida gani kuwa Myahudi?
b. Kwa kila njia! Paulo anajua kuna faida nyingi ambazo Mungu aliwapa Wayahudi. Hasa, aliwakabidhi maneno ya Mungu, ambayo yanazungumza juu ya ufunuo ulioandikwa wa Mungu kabla ya wakati wa Yesu. Aliwapa watu wa Kiyahudi neno lake, na hiyo ni zawadi isiyoelezeka.
i. “Hili lilikuwa pendeleo lao kuu, walikuwa watunza-maktaba wa Mungu, hazina hii ya kimbingu ilikubaliwa kwao.” (Trapp)
ii. Paulo baadaye ataeleza faida ya watu wa Kiyahudi katika Warumi 9:4, akieleza kwamba Israeli pia walikuwa wana, utukufu, maagano, utoaji wa sheria, utumishi wa Mungu, na ahadi.
2. (3–4) Kutokuamini kwa Kiyahudi hakumfanyi Mungu kuwa na makosa.
Na kama wengine hawakuamini? Je, kutokuamini kwao kutafanya uaminifu wa Mungu kuwa bure? Hakika sivyo! Hakika acha Mwenyezi Mungu awe mkweli na kila mtu ni mwongo, kama ilivyoandikwa.
“Ili upate kuhesabiwa haki katika maneno yako,
Na upate kushinda uhukumiwapo.
a. Na je ikiwa wengine hawakuamini? Ukweli wayaudi kwa ujumla wao walikuwa wameikataa injili haikumaanisha uaminifu wa Mungu kwao ulikuwa bure. Haikumaanisha kazi ya Mungu ilikuwa bure au haina matokeo.
i. “Ni seme na Paulo, ‘Itakuwaje ikiwa wengine hawakuamini? Si jambo jipya; daima kumekuwa na baadhi ambao wamekataa ufunuo wa Mungu. Kwa hivyo? Afadhali wewe na mimi tuendelee kuamini, na kujijaribu wenyewe, na kuthibitisha uaminifu wa Mungu, na kuishi kwa ajili ya Kristo Bwana wetu, ingawa tunaona kundi lingine la watu wenye mashaka, na wengine, na mwingine hali bila kipimo. Injili haipungukiwi, kama wengi wetu tunavyojua.” (Spurgeon)
b. Hakika sivyo! Hakika, Mungu awe kweli lakini kila mtu mwongo: Paulo anatukumbusha Mungu atahesabiwa haki katika matendo yake yote. Mwishowe, itadhihirika hata udhalimu wetu kwa namna fulani utatangaza haki yake na utukufu wake, hata ikiwa katika hukumu.
i. “Mtu akisema ahadi ya Mungu haijatimia kwake, na auchunguze moyo wake na njia zake, atagundua kuwa ameiacha njia ile ambayo Mungu peke yake angeweza kuitimiza ahadi yake, kwa utakatifu na kweli yake. (Clarke)
ii. Spurgeon acha Mungu awe wa kweli lakini kila mtu mwongo: “Ni maneno ya ajabu, yenye nguvu; lakini haina nguvu. Ikiwa Mungu anasema jambo moja, na kila mtu katika ulimwengu akasema lingine, Mungu ni wa kweli, na watu wote ni waongo. Mungu anasema ukweli, na hawezi kusema uwongo. Mungu hawezi kubadilika; neno lake, kama yeye mwenyewe, halibadiliki. Tunapaswa kuamini ukweli wa Mungu ikiwa hakuna mtu mwingine anayeuamini. Makubaliano ya jumla ya maoni si kitu kwa Mkristo. Anaamini neno la Mungu, na anafikiria zaidi kuliko maoni ya watu wote.”
3. (5) Pingamizi kuhusu udhalimu wa mwanadamu na haki ya Mungu.
Ikiwa uovu wetu wadhihirisha haki ya Mungu, tuseme nini? Mungu ni dhalimu anayeleta ghadhabu? (Nazungumza kama mwanaume.)
a. Ikiwa uovu wetu unadhihirisha haki ya Mungu, tutasema nini? Paulo analeta hoja ya kupingana na mpinzani: “Ikiwa udhalimu wangu utaonyesha haki ya Mungu, Mungu atanihukumuje? Dhambi yangu hatimaye hutumika kumletea utukufu zaidi, na ni vyema!”
b. Je! Mungu ni dhalimu anayeleta ghadhabu? Paulo alifahamu mstari wa kufikiri unaosema, “Mungu ndiye anayetawala kila kitu. Hata uovu wangu hatimaye utaonyesha haki yake. Kwa hiyo Mungu yu dhalimu akiniwekea ghadhabu yake, kwa sababu mimi ni rungu mkononi mwake.”
i. Kwa nadharia, mfano wa kushangaza zaidi wa mtu anaweza kuuliza swali hili ni Yuda. Unamsikia Yuda akitoa hoja yake? “Bwana, najua nilimsaliti Yesu, lakini uliitumia kwa wema. Kwa kweli, kama singefanya nilichofanya, Yesu asingeenda msalabani hata kidogo. Nilichofanya hata kilitimiza Maandiko. Unawezaje kunihukumu ?” Jibu kwa Yuda linaweza kuwa hivi: “Ndiyo, Mungu alitumia uovu wako lakini bado ulikuwa uovu wako. Hukuwa na nia njema au safi moyoni mwako hata kidogo. Si sifa kwako Mungu alileta mema katika uovu wako. Unasimama kwa hatia mbele za Mungu.”
c. Nazungumza kama mwanadamu: Hii haimaanishi Paulo hana uvuvio wa Roho Mtakatifu na mamlaka ya kitume. Badala yake anaeleza kama mwanadamu tu – mtu aliyeanguka wakati huo – mtu yeyote anaweza kuthubutu kuhoji haki ya Mungu.
4. (6–8) Jibu la Paulo kwa pingamizi lililotolewa.
Sivyo! Mungu atauhukumuje ulimwengu? ikiwa kweli ya Mungu imeongezeka kwa njia ya uongo wangu hata kupata utukufu wake, kwa nini mimi pia nihukumiwe kuwa mwenye dhambi? Na kwa nini tusiseme, “Tufanye maovu ili mema yaje”?; kama tunavyoshutumiwa na wanavyosisitiza tunasema. Hukumu yao ni ya haki.
a. Hakika sivyo! Mungu atauhukumuje ulimwengu? Paulo anatupilia mbali swali la mpinzani wake kwa urahisi. Ikiwa mambo yangekuwa kama vile mpinzani wake alivyopendekeza, basi Mungu asingeweza kumhukumu yeyote.
i. Ni kweli Mungu atatumia udhalimu wa mwanadamu kukamilisha kazi Yake na kuleta sifa kwa jina Lake – usaliti wa Yuda kwa Yesu ni mfano kamili. Hata hivyo, sehemu ambayo Mungu hujitukuza katika dhambi ya mwanadamu ni kwa kuhukumu udhalimu huo kwa uadilifu.
b. Mungu atauhukumuje ulimwengu? Kwa wote wawili Paulo na wasomaji wake ilitolewa siku ya hukumu ilikuwa inakuja, wakati wengine wataachiliwa na wengine kuhukumiwa. Hakuhitaji kupinga hatua hii; ilieleweka tu katika utamaduni huo.
i. Paulo alielewa Mungu angehukumu ulimwengu, Wayahudi na Wamataifa. Wayahudi wengi wa siku za Paulo walifikiri Mungu angemhukumu Mmataifa kwa ajili ya dhambi yake, lakini kuokoa Myahudi licha ya dhambi yake.
c. Ikiwa ukweli wa Mungu umeongezeka kwa njia ya uongo wangu na kupata utukufu wake, kwa nini mimi nihukumiwe kama mwenye dhambi? Paulo anarudia pingamizi la muulizaji wa kuwaziwa: “Ikiwa Mungu atajitukuza kwa uongo wangu, atanihukumuje, na ninaonekana kuongeza utukufu wake kwa njia isiyo ya moja kwa moja?
d. Tutende maovu ili mema yaje: Huu ulikuwa ni upotoshaji wa fundisho la Paulo la kuhesabiwa haki kwa imani, na nyongeza ya pingamizi la muulizaji wake wa dhana. Ukitafakari zaidi kuhusu wazo la adui wa Paulo mbali vya kutosha, unaishia kusema, “Tutende dhambi kadiri tuwezavyo ili Mungu atukuzwe hata zaidi.” Hii inatuonyesha njia moja ya kuchunguza fundisho ni kupanua maana na matokeo yake na kuona mahali unaishia.
i. Bila shaka, tufanye maovu ili mema yaje, hayakuwa mafundisho ya Paulo. Aliripotiwa kwa kashfa kufundisha hili. Bado, inawezekana kuona jinsi shtaka hili lilivyokuja wakati Paulo alihubiri kwa huru msamaha na wokovu kwa neema nanjia ya imani katika Yesu, si matendo.
ii. Mahubiri mengi ya Kikristo yako mbali sana na injili ya kweli ya neema ya bure ambayo Paulo alihubiri hakuna njia ambayo mtu yeyote angeweza kuripoti kwa uchongezi walifundisha “tufanye maovu ili mema yaje.” Iwapo tunajikuta wakati fulani tunashutumiwa kuhubiri injili “iliyo wazi sana” na inayozingatia sana imani na neema na kazi ya Mungu basi tunajikuta katika ushirika mzuri na Paulo.
e. Hukumu yao ni ya haki: Paulo hatajibu upotoshaji huo wa kipuuzi wa injili yake. Anasema tu juu ya wale ambao wangefundisha mambo kama hayo au kumshtaki Paulo kwa kuwafundisha, hukumu yao ni ya haki. Mungu humhukumu kwa haki mtu yeyote anayefundisha au kuamini jambo kama hilo.
i. Kupindisha kipawa cha bure cha utukufu wa Mungu katika Yesu kuwa kibali kinachodhaniwa cha kufanya dhambi ndicho kilele cha upotovu wa mwanadamu. Inachukua zawadi nzuri zaidi ya Mungu na kuipotosha na kuidhihaki. Upotoshaji huu ni wa dhambi Paulo anauokosoa mwishoni, kwa sababu ni zaidi ya upotovu wa wapagani (Warumi 1:24–32), zaidi ya unafiki wenye maadili (Warumi 2:1–5), na zaidi ya imani potofu ya Myahudi (Warumi 2:17–29).
B. Hitimisho: upotovu wa kijumla kwa wanadamu wote mbele za Mungu.
1. (9) Hatia ya Myahudi na Myunani mbele za Mungu.
Je! sisi ni bora kuliko wao? Hapana kabisa. Kwa maana hapo awali tuliwashtaki Wayahudi na Wayunani wote wako chini ya dhambi.
a. Je, sisi ni bora kuliko wao? Sivyo kabisa: Kwa kuwa Paulo alikuwa Myahudi kwa kuzaliwa na kurithi (Wafilipi 3:4–6), anaposema “sisi” anamaanisha “sisi Wayahudi.” Ukweli ni kwa asili, mtu wa Kiyahudi hana haki tena mbele ya Mungu kuliko mpagani au mwadilifu. Paulo anaonyesha wapagani, wenye maadili mema, na Wayahudi wote wako chini ya dhambi na chini ya hukumu.
b. Chini ya dhambi: Hii ni kauli yenye nguvu. Inazungumza juu ya utumwa wetu wa dhambi, maana yake kihalisi “kuuzwa chini ya dhambi.” Kwa asili kila mtu anajua jinsi kuwa mtumwa wa dhambi, Wayahudi na Wagiriki.
i. Chini ya nguvu ya dhambi, lakini zaidi chini ya hatia ya dhambi.(Poole)
ii. Morris chini ya dhambi: “Anaiona dhambi kama mtawala dhalimu, ili wenye dhambi wawe ‘chini’ yake ( Biblia ya yerusalemu, ‘chini ya utawala wa dhambi’); hawawezi kuondoka wakiwa huru.”
2. (10–18) Agano la Kale linashuhudia upotovu wa ulimwengu wote na hatia ya wanadamu.
Kama ilivyoandikwa:
“Hakuna mwenye haki, hata mmoja;
Hakuna afahamuye;
Hakuna afahamuye; anamtafuta Mungu.
Wote wamepotoka;
Wote pamoja wamekuwa bila faida;
Hakuna atendaye mema, hakuna hata mmoja”.
“Koo lao ni kaburi lililowazi;
Kwa ndimi zao wametenda hila”;
“Sumu ya nyoka i chini ya midomo yao”;
“Ambao vinywa vyao vimejaa laana na uchungu.”
“Miguu yao ina wepesi kumwaga damu;
Uharibifu na taabu zimo katika njia zao;
Na njia ya amani wanaitafuta. hawajaupata.”
“Hamna kumcha Mungu mbele ya macho yao.”
a. Hakuna mwenye haki, hakuna, hata mmoja: Nukuu hizi kutoka Zaburi (Zaburi 14:1–3; 5:9, 140:3, 10:7 na 36:1) na kutoka Isaya 59:7–8 zote zinaunga mkono taarifa hii ya ufunguzi.
i. Paulo anaangalia hali ya kibinadamu kutoka juu hadi chini. Anaanza na kichwa na huenda chini kwa miguu. Warren Wiersbe anakiita kifungu hiki “Uchunguzi wa uyoka wa mwenye dhambi aliyepotea, kutoka kichwa hadi mguu.”
ii. Mtazamo huu wa hali ya kibinadamu unasikitisha. Kuna maana gani? Mtume Paulo anatutaka tuelewe kutoweza kwetu kabisa kujiokoa. Anguko linagusa kila sehemu ya utu wa mwanadamu, na hesabu ya viungo vya mwili vilivyoharibiwa na anguko hudhihirisha hili.
b. Hakuna mwenye haki, hata mmoja: Mungu asipompata mwenye haki, ni kwa sababu hakuna hata mmoja. Sio kwamba kuna wengine na Mungu hakuweza kuwaona. Hakujawai kuwa na mtu mwenye haki, isipokuwa Yesu Kristo. “Hata Adamu hakuwa mwadilifu, hakuwa na hatia – pasipo kujua mema na mabaya.” (Newelli)
c. Hakuna amtafutaye Mungu: Tunajidanganya kwa kufikiri mwanadamu, peke yake, anamtafuta Mungu. Lakini je, dini zote na mila na desturi tangu mwanzo wa nyakati hazionyeshi mwanadamu anamtafuta Mungu? La hasha. Mwanadamu akianzisha utafutaji basi hatafuti Mungu wa kweli, Mungu wa Biblia. Badala yake anatafuta sanamu anayojitengenezea.
i. “Mmepitia aina hii ya ibada, lakini hamjamtafuta Mungu. Ninaumwa na udini huu mtupu. Tunauona kila mahali; sio ushirika na Mungu, sio kumfikia Mungu, hakika Mungu hayupo hapo hata kidogo.” (Spurgeon)
d. Pamoja wamekuwa wasio na faida: Neno lisilofaa lina wazo la tunda iliyooza. Inazungumza juu ya kitu kilichokuwa kibaya na kwa hivyo hakifai.
e. Koo lao ni kaburi lililo wazi: Kwa marejeo haya kutoka katika Zaburi, Paulo anaita sehemu ya mwili wa mwanadamu katika hatia. Koo, ulimi, midomo, kinywa, miguu, na macho yamejaa dhambi na uasi dhidi ya Mungu.
i. Miguu yao ni nyepesi kwa kumwaga damu: Kwa maelezo zaidi, soma karatasi zako za kila siku (Newelli). Kwa kielelezo, Los Angeles Times liliripoti 1992 mauaji yalifikia kiwango cha rekodi cha 800 katika jimbo la Los Angeles.
f. Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yao: Hii ni muhtasari wa wazo zima. Kila dhambi na uasi dhidi ya Mungu hutokea kwa sababu hatuna heshima ifaayo kwake. Popote palipo na dhambi, hakuna kumcha Mungu.
i. John Calvin juu ya kumcha Mungu: “Kwa kifupi, kama vile ni hatamu kuzuia uovu wetu, hivyo inapopungua, tunahisi tuko huru kujiingiza katika kila aina ya ufisadi.”
3. (19–20) Muhtasari: torati haiwezi kutuokoa kutoka kwa dhambi zetu na adhabu inayostahili.
Tunajua ya kuwa lolote inenayo torati, inawaambia hao walio chini ya sheria, ili kila kinywa kifungwe, na ulimwengu wote unaweza kuwa na hatia mbele za Mungu. Kwa hiyo hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria, kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.
a. Chochote ambacho sheria inasema: Paulo anaonyesha maelezo haya ya kutisha ya dhambi ya mwanadamu yanatujia katika sheria; na inakusudiwa kwa wale walio chini ya sheria, kumnyamazisha kila mkosoaji na kudhihirisha hatia ya wanadamu wote – ili ulimwengu wote uwe na hatia mbele za Mungu.
i. “Tunaweza kuongeza, ingawa maovu yote yaliyoorodheshwa hapa hayapatikani waziwazi kwa kila mtu, lakini yanaweza kuhusishwa kwa haki na kweli kwa asili ya mwanadamu, kama tulivyoona.’’ (Calvin)
b. Inasema kwa wale walio chini ya sheria, Ikiwa Mungu anasema hivi juu ya wale walio na sheria, na kujaribu kuitii, ni dhahiri hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria.
i. Kumbuka Wayahudi wengi wa siku za Paulo walichukua kila kifungu cha Agano la Kale kinachoelezea uovu na kukitumia kwa watu wa mataifa pekee – sio kwao wenyewe. Paulo anaweka wazi Mungu husema na wale walio chini ya sheria.
c. Kwa hiyo hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki kwa matendo ya sheria mbele zake: sheria haiwezi kutuokoa. Sheria haiwezi kuhalalisha mtu yeyote. Yafaa katika kutupa elimu ya dhambi, lakini haiwezi kutuokoa kutoka kwalo.
i. Tangu wakati wa Adamu na Hawa, watu wamejaribu kujihesabia haki kwa matendo ya sheria. Katika bustani ya Edeni Adamu alijaribu kujifanya aonekane mkamilifu mbele za Mungu kwa kutengeneza vifuniko kutoka kwa matawi ya mtini – na alishindwa. Katika Ayubu, kitabu cha kale zaidi cha Biblia, tatizo limewasilishwa kwa uwazi: mtu anawezaje kuwa mwenye haki mbele za Mungu? (Ayubu 9:2). Mungu anaweka wazi sehemu ya jibu hapa kupitia Paulo – jibu si katika utendaji wa matendo mema, katika matendo ya sheria.
ii. Jinsi tunavyohitaji kuelewa hili kwa undani – kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki!
∙Hii ina maanisha sheria, baada ya kuvunjwa, sasa inaweza tu kutuhukumu – haiwezi kutuokoa kamwe.
∙ Hii ina maanisha hata kama tungeweza kwa sasa kuanza kuishika sheria ya Mungu kikamilifu haiwezi rekebisha uasi wa wakati uliopita, au kuondoa hatia ya sasa.
∙ Hii ina maana kwamba kushika sheria si njia ya Mungu ya wokovu au ya baraka chini ya Agano Jipya.
d. Kwa sheria ni ufahamu wa dhambi: ufafanuzi wa JB Phillip wa kifungu hiki ni ya kushangaza. Anaandika, “ni ncha iliyonyooka ya Sheria ndiyo inayotuonyesha jinsi tulivyo wapotovu.”
i. Ili mtu yeyote asifikirie kuwa sheria hiyo haina maana, anaendelea kuonyesha matumizi yake, lakini kinyume kabisa na kile walichokusudia.(Poole)
C. Ufunuo wa haki ya Mungu.
1. (21) Ufunuo wa haki.
Lakini sasa, haki ya Mungu pasipo sheria imedhihirishwa, inashuhudiwa na torati na manabii,
a. Lakini sasa: Maneno haya yanatoa mpito tukufu zaidi kutoka kwa hukumu ya Warumi 3:20 hadi kuhesabiwa haki kwa Warumi 3:21.
i. Lakini sasa inazungumza juu ya upya wa kazi ya Mungu katika Yesu Kristo – hakika ni Agano Jipya. Kushuhudiwa kwa Sheria na Manabii kunatukumbusha kuna mwendelezo wa kazi ya Mungu katika nyakati za zamani.
b. Kando na sheria: Sheria haiwezi kutuokoa, lakini Mungu anadhihirisha haki ambayo itatuokoa, kando na sheria. Hiki ndicho kiini cha mpango wa Mungu wa wokovu katika Yesu Kristo. Ni wokovu unaotolewa mbali na sheria, mbali na mapato yetu wenyewe na tunayostahili, mbali na mastahili yetu wenyewe.
c. Kushuhudiwa na Sheria na Manabii: Uadilifu huu si jambo geni. Paulo “hakuivumbua”. Ilitabiriwa zamani sana, ikishuhudiwa na Torati na Manabii. Agano la Kale lilisema haki hii inakuja.
d. Kando na sheria: Sio haki ya Mungu imefunuliwa mbali na Agano la Kale, lakini inafunuliwa mbali na kanuni ya sheria. Ni mbali na uhusiano wa kisheria na Mungu, unaotokana na wazo la kupata na kustahiki sifa mbele zake.
i. “Kiyunani huweka mbele kabisa kifungu hiki kikuu cha maneno mbali na sheria (choris nomou) na hii inaweka wazi kabisa utengano kamili wa haki hii ya Kimungu na utendakazi wowote wa sheria, kazi zozote za mwanadamu, kwa vyovyote vile.” (Newelli)
ii. Haki ya Mungu haitolewi kwetu kama kitu cha kuchukua ulegevu kati ya uwezo wetu wa kushika sheria na kiwango kamili cha Mungu. Haijatolewa ili kuongeza haki yetu wenyewe, inatolewa mbali kabisa na haki yetu ulio jaribiwa.
2. (22) Jinsi haki hii inavyowasilishwa kwa mwanadamu.
Haki hiyo ya Mungu kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote na juu ya wote waaminio. Maana hakuna tofauti;
a. Kwa wote na juu ya wote wanaoamini: Katika Warumi 3:21, Paulo alituambia jinsi haki hii haikuji. Haikuji kwa matendo ya sheria, ni mbali na sheria. Sasa Paulo anatuambia jinsi haki hii ya kuokoa inavyokuja. Ni kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote na juu ya wote waaminio.
b. Kwa njia ya imani katika Yesu Kristo: Haki ya Mungu si yetu kwa imani, ni yetu kupitia imani. Hatupati haki kwa imani yetu. Tunapokea haki kupitia imani katika Yesu Kristo.
i. Kupitia imani “inaelekeza kwenye ukweli kwamba imani si sifa, kupata wokovu. Si zaidi ya njia ambayo zawadi inatolewa.” (Morris)
ii. “Lakini imani si ‘kuamini’ au ‘kutarajia’ Mungu kufanya jambo fulani, bali kutegemea ushuhuda wake kuhusu nafsi ya Kristo kama Mwana wake, na kazi ya Kristo kwa ajili yetu msalabani… Baada ya imani kuokoa, maisha ya uaminifu huanza… uaiminifu kunatazamia kila mara kile ambacho Mungu atafanya; lakini imani huona kile anachosema Mungu kimetendeka, na kuliamini neno la Mungu, tukiwa na hakika ni kweli, na kweli kwetu sisi wenyewe.” (Newelli)
c. Kwa maana hakuna tofauti: Hakuna njia nyingine ya kupata haki hii. Haki hii haipatikani kwa kuitii sheria; ni haki inayopokelewa, ipatikanayo kwa imani katika Yesu Kristo.
i. “Kuna kitabu kidogo chenye mada, Kila mtu wakili mwenyewe. Naam, siku hizi, kulingana na baadhi ya watu, inaonekana kila mtu anapaswa kuwa mwokozi wake binafsi; lakini kama ningekuwa nayo, sema; injili kadhaa, na ingenibidi kuzitatua, na kutoa injili sahihi kwa mtu anayefaa, ni marekebisho gani niliyopaswa kuwa nayo! Ninaamini, mara nyingi, ninapaswa kuwa natoa injili yako kwa mtu mwingine, na injili ya mtu mwingine kwako; na yote yangekuwa machafuko kiasi gani! Lakini sasa tuna tiba moja ya ulimwengu wote… Damu na haki ya Yesu Kristo itamwokoa kila mtu anayemwamini, ‘hakuna tofauti.’” (Spurgeon)
3. (23–24) Hitaji la kijumla la mwanadamu ulimwenguni kote na toleo la Mungu la ulimwengu wote.
Kwa maana wote wametenda dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu, wakihesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Yesu Kristo,
a. Kuhesabiwa haki:Paulo anaendeleza mafundisho yake kuhusu wokovu katika mambo matatu.
∙ Kuhesabiwa haki ni taswira kutoka mahakama ya sheria.
∙ Ukombozi ni pichataswira kutoka soko la watumwa.
∙ Upatanisho ni taswira kutoka kwa ulimwengu wa dini, kumpendeza Mungu kwa dhabihu.
i. Kuhesabiwa haki kunatatua tatizo la hatia ya mwanadamu mbele ya Hakimu mwadilifu. Ukombozi unatatua tatizo la utumwa wa mwanadamu kwa dhambi, ulimwengu na shetani. Upatanisho hutatua tatizo la kumchukiza Muumba wetu.
b. Wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu: Kauli hii ya ulimwengu wote inajibiwa na toleo la ulimwengu wote la kuhesabiwa haki bure kwa neema yake. Iko wazi kwa kila atakayeamini.
i. Morris, akimnukuu Moule: “Kahaba, mwongo, muuaji, wamepungukiwa nayo; na hata wewe. Labda wanasimama chini ya mgodi, na wewe kwenye kilele cha Alp; lakini hauwezi hata kidogo kama wao kuziguza nyota.” Kila mtu hupungukiwa, kila mtu anaweza kuhesabiwa haki bure kwa neema yake.
c. Kupungukiwa na utukufu wa Mungu: Haiwezekani kueleza kila njia tunayopungukiwa, lakini hapa kuna njia nne muhimu mwanadamu anapungukiwa na utukufu wa Mungu.
i. Tunashindwa kumpa Mungu utukufu unaomstahili, kwa maneno, mawazo na matendo yetu.
ii. Tunashindwa kustahili, na hivyo kukataa utukufu na thawabu ambayo Mungu huwapa watumishi waaminifu.
iii. Tunashindwa kuakisi utukufu wa Mungu ipasavyo kwa kukataa kufanana na mfano wake.
iv. Tunashindwa kupata utukufu wa mwisho ambao Mungu atawapa watu wake mwisho wa historia yote.
d. Kuhesabiwa haki bure kwa neema yake: kuwa katika hali hiyo ya dhambi, njia pekee ya sisi kuhesabiwa haki ni kuhesabiwa haki bure. Hatuwezi kuinunua kwa kazi zetu nzuri hata kidogo. Ikiwa haijawekwa bure kwetu, hatuwezi kuwa nayo. Kwa hivyo tunahesabiwa haki kwa bure kwa neema Yake – kibali chake kisichostahiliwa, tulichopewa bila kuzingatia kile tunachostahili. Ni utoaji unaohamasishwa tu na mtoaji, na hauchochewi na chochote katika yule anayepokea.
i. Bure ni neno la kale la Kiyunani dorean. Jinsi neno hili linavyotumika katika vifungu vingine vya Agano Jipya hutusaidia kuelewa neno hilo. Mathayo 10:8 (Mmepokea bure, toeni bure) na Ufunuo 22:17 (Na yeyote anayetaka, na ayatwae maji ya uzima bure) huonyesha kwamba neno hilo linamaanisha bure kweli, si “gharama nafuu” au “punguzo tu.” Labda matumizi ya kuvutia zaidi ya neno la kale la Kiyunani dorean ni katika Yohana 15:25: Walinichukia bila sababu (dorean). Hata kama vile hakukuwa na chochote ndani ya Yesu kinachostahili kuchukiwa na mwanadamu, vivyo hivyo hakuna ndani mwetu chochote kinachostahili kuhesabiwa haki – sababu zote ziko kwa Mungu.
ii. Calvin juu ya matumizi ya maneno yote mawili kwa uhuru na neema: “Hivyo anarudia neno ili kuonyesha yote yanatoka kwa Mungu, na hakuna kutoka kwetu… maana yake kwa kurudiarudia, na kudai ni kwa rehema ya Mungu pekee utukufu wote wa haki yetu.”
e. Kupitia ukombozi ulio katika Kristo Yesu: Injili ya Paulo tena inajikita kikamilifu katika Kristo Yesu. Wokovu unawezekana kwa ukombozi unaopatikana ndani yake. Mungu hawezi kutupa haki Yake isipokuwa Yesu Kristo.
f. Ukombozi: Hili lina wazo la kurudisha kitu, na linahusisha gharama. Hata hivyo, Mungu hulipa gharama na hivyo tunahesabiwa haki bure.
i. Neno lililotafsiriwa ukombozi lilikuwa na asili yake ikieleza kuachiliwa kwa wafungwa wa vita kwa malipo ya bei na lilijulikana kuwa “fidia.” Kadiri muda ulivyosonga, iliongezwa ili kujumuisha kuachiliwa kwa watumwa, tena kwa malipo.
ii. Wazo la ukombozi maana yake ni Yesu alitununua; kwa hiyo, sisi ni wake. Paulo alionyesha wazo hili katika barua nyingine: Mlinunuliwa kwa thamani; basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu na roho zenu ambazo ni za Mungu (1 Wakorintho 6:20).
4. (25–26) Jinsi kifo cha Yesu kinatosheleza hukumu ya haki ya Mungu.
Yeye ambaye Mungu amekwisha mweka awe patanisho na damu yake, kwa njia ya imani, ili aonyeshe haki yake; kwa unyenyekevu wake Mungu alimwekelea dhambi ulio tendwa, ili aonyeshe haki yake wakati huu, apate kuwa mwenye haki, na mwenye kumhesabia haki yeyote amwaminiye Yesu.
a. Ambaye Mungu alimweka kama upatanisho: Yesu, kwa kifo chake (kwa damu yake) alikuwa patanisho (dhabihu badala ya) kwa ajili yetu. Jinsi alivyohukumiwa badala yetu, Baba angeweza kuonyesha haki yake katika hukumu dhidi ya dhambi, huku akiwaachilia wale waliostahili hukumu.
i. Wuest juu ya upatanisho: “Neno katika hali yake ya kitambo lilitumika kwa tendo la kuridhisha miungu ya Kigiriki kwa dhabihu… kwa maneno mengine, dhabihu ilitolewa ili kuikomboa hasira ya mungu.”
ii. NIV inatafsiri upatanisho kama dhabihu ya upatanisho; Biblia Hai: kuchukua adhabu ya dhambi zetu.
b. Upatanisho: Neno la kale la Kigiriki la upatanisho (hilasterion) linatumiwa pia katika barua nyingine kumaanisha kiti cha rehema, kifuniko kinachofunika Sanduku la Agano, ambacho juu yake damu ya dhabihu ilinyunyiziwa kama upatanisho kwa ajili ya dhambi. Ingawa inaweza kusemwa kifungu hiki kinamaanisha “Yesu ndiye kiti chetu cha rehema,” pengine lina wazo la moja kwa moja la upatanisho – dhabihu badala.
i. Wakati uo huo, wazo la kiti cha rehema halipaswi kupuuzwa kama kielelezo cha upatanisho. Ndani ya Sanduku la Agano kulikuwa na ushahidi wa dhambi kuu ya mwanadamu: mbao za sheria; mana walipokea bila shukrani; fimbo ya Haruni iliyochipuka, ikionyesha uasi wa mwanadamu dhidi ya uongozi wa Mungu. Juu ya Sanduku la Agano kulikuwa na alama za uwepo mtakatifu wa Mungu aliyeketishwa ndani ya makerubi wazuri wa dhahabu. Katikati ya vile viwili vilisimama kiti cha rehema, na damu ya dhabihu iliponyunyiziwa juu ya kiti cha rehema katika Siku ya Upatanisho (Mambo ya Walawi 16), ghadhabu ya Mungu iliepukwa kwa sababu mbadala, alikuwa ameuawa kwa niaba ya wenye dhambi waliokuja kwa imani. Kwa kweli tunaweza kusema Yesu ndiye “kiti chetu cha rehema,” akisimama kati ya wenye dhambi wenye hatia na utakatifu wa Mungu.
c. Ambaye Mungu alimweka kuwa upatanisho: Hili linaonyesha Yesu hakumtuliza kwa njia fulani Baba aliyesitasita, hataki kuzuia ghadhabu Yake. Badala yake, Mungu Baba ndiye aliyeanzisha upatanisho: ambaye Mungu alimweka.
d. Kupita juu dhambi: Mungu, katika ustahimilivu wake, alikuwa amepita juu ya dhambi za wale watakatifu wa Agano la Kale waliomwamini Masihi ajaye. Msalabani dhambi hizo hazikupitishwa tena, bali zililipwa.
i. Wazo ni kupitia dhabihu ya wanyama katika Agano la Kale, wale waliotazamia kwa imani kwa Masihi ajaye dhambi zao “zilifunikwa” na aina ya “IOU” au barua ya ahadi isiyo badilika. Kifuniko hicho cha muda kilikombolewa kwa malipo kamili msalabani.
ii. Kazi ya Yesu msalabani ilimweka Mungu kutoka kwa shtaka kuwa alipitisha kidogo dhambi iliyotendwa mbele ya msalaba. Dhambi hizo zilipitishwa kwa muda lakini hatimaye zililipwa.
e. Ili apate kuwa mwenye haki na mwenye kumhesabia haki yeyote amwaminiye Yesu: Msalabani, Mungu alidhihirisha haki yake kwa kumpa mwanadamu kuhesabiwa haki (hukumu ya kisheria uio badilika ya “kutokuwa na hatia”), huku akibaki kuwa mwenye haki kabisa (kwa sababu adhabu ya haki ya dhambi ilikuwa imelipwa msalabani).
i. Ni rahisi kuona jinsi mtu anavyoweza kuwa mwenye haki tu – kumpeleka tu kila mwenye dhambi mwenye hatia kuzimu, kama hakimu mwenye haki angefanya. Ni rahisi kuona jinsi mtu anavyoweza kuwa mwadilifu – mwambie kila mwenye dhambi mwenye hatia, “Ninatangaza msamaha. Nyote mmetangazwa ‘hamna hatia.’” Lakini ni Mungu pekee angeweza kupata njia ya kuwa zote mwenye haki na mwenye kuhesabia haki yule aliye na imani katika Yesu.
ii. “Hapa tunajifunza Mungu alikusudia kutoa maonyesho yaliyo wazi zaidi ya haki na rehema yake. Ya haki yake, katika kuhitaji dhabihu, na kukataa kabisa kutoa wokovu kwa ulimwengu uliopotea kwa njia nyingine yoyote; na rehema zake, katika kutoa dhabihu ambayo haki yake ilihitaji.” (Clarke)
5. (27) Kujisifu katika wokovu unaokuja kwa njia ya injili ya Yesu Kristo haku jumuishwa.
Kujisifu ku wapi basi? kumetengwa. Kwa sheria gani? Ya kazi? La, bali kwa sheria ya imani.
a. Kujisifu ku wapi basi? Hakupaswi kuwa popote. Kwa sababu tunahesabiwa haki bure kwa neema yake, hakuna nafasi ya kujipongeza au kujisifu.
b. Kwa sheria gani? Majivuno na kiburi havijatengwa kwa sababu kuna kifungu maalum katika sheria dhidi yazo. Badala yake, kiburi hakijumuishwi kwa sababu hakipatani kabisa na wokovu ambao ni wetu bure kwa imani. Kujisifu kunaondolewa na sheria ya imani.
c. Kwa sheria ya imani: Hakuna nafasi ya kujisifu! Hii ndiyo sababu mwanadamu wa asili anachukia kuhesabiwa haki bure kwa neema yake. Neema yanakataa kabisa kutambua sifa zake (zinazowaziwa) na haitoi nafasi kwa kiburi chake hata kidogo.
6. (28–30) Kuhesabiwa haki (kuachiliwa katika mahakama ya Mungu) hupatikana, kwa Myahudi na Myunani, pasipo matendo ya sheria.
Basi twaona ya kuwa mtu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria. Ama yeye ni Mungu wa wayahudi tu? Je, yeye si Mungu wa Mataifa pia? Naam, wa Mataifa pia, kwa kuwa Mungu ni mmoja, atakayewahesabia haki waliotahiriwa kwa imani, na wale wasiotahiriwa kwa imani.
a. Tunahesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria: si kwamba tunahesabiwa haki kwa imani pamoja na matendo yo yote ya sheria tunayoweza kufanya. Tunahesabiwa haki kwa imani pekee, pasipo matendo ya sheria.
i. “Kwa kuwa matendo yote ya sheria yamezuiliwa, imani peke yake imesalia. Luther alitafsiri hivyo, na tangu wakati wake Sola Fide imekuwa wito.” (Lenski)
b. Mbali na matendo ya sheria: Je, Yakobo hapingani na hili katika vifungu Yakobo 2:14–26? Tunawezaje kusema kwamba ni imani pekee ndiyo iokoayoinayookoa, pasipo matendo ya sheria?
i. Ni imani ya kweli pekee ndiyo inayookoa, lakini imani ya kweli, imani inayookoa, ina sifa tofauti. Sio kukubaliana na mambo fulani tu, bali ni kuelekeza akili na mapenzi kwa kupatana na Mungu. Kusudi zima la kitabu cha Yakobo ni kuelezea tabia ya imani hii iokoayo.
ii. Calvin aeleza hivi: “Yakobo anaposema, kwamba mwanadamu hahesabiwi haki kwa imani pekee, bali pia kwa matendo, hapingi hata kidogo maoni yaliyotangulia [ya kuhesabiwa haki kwa imani pekee]. Upatanisho wa maoni hayo mawili unategemea hasa kulegeza kwa hoja inayofuatwa na Yakobo. Swali kwake si jinsi watu wanavyopata haki mbele za Mungu, bali jinsi wanavyothibitisha kwa wengine wanahesabiwa haki; lengo lake lilikuwa kuwashindanisha wanafiki, ambao walijisifu bure walikuwa na imani… Yakobo hakumaanisha zaidi ya kwamba mtu hafanywi au kuthibitishwa kuwa mwadilifu kwa imani ya kujifanya au mfu, lazima athibitishe haki yake kwa matendo yake.”
c. Ndiyo, ya watu wa mataifa pia: Haki hii inatolewa kwa Myahudi na Myunani pia. Tabia ya ulimwengu wote ya toleo hilo inaonyeshwa na ukweli rahisi: Je, Yeye si Mungu wa Mataifa pia? Bila shaka yuko. Ikiwa kuna Mungu mmoja tu, basi Mungu ni Mungu wa Mataifa kama vile Yeye ni Mungu wa Wayahudi. Ni juu ya Mataifa tu kumtambua kuwa Mungu.
d. Kuna Mungu mmoja ambaye atawahesabia haki wale waliotahiriwa kwa imani na wale wasiotahiriwa kwa njia ya imani: Sio tu kwamba haki hii inapatikana kwa Wayahudi na Wamataifa, bali pia inapokelewa kwa njia hiyo na Wayahudi na Wamataifa. Mungu huhesabia haki Myahudi na Myunani, yeye huwahesabia haki hivyo: kwa imani… kupitia imani.
7. (31) Je! nilipi basi sheria?
Je, twaibatilisha sheria kwa imani? Hakika sivyo! Kinyume chake, tunaweka sheria.
a. Je, twaibatilisha sheria kwa imani? Tunaweza kuona jinsi mtu anavyoweza kuuliza, “Kama sheria haitufanyi kuwa waadilifu, inafaa nini? Paulo, umeibatilisha sheria. Unaenda kinyume na sheria ya Mungu.”
b. Hakika sivyo! Bila shaka, Paulo habatilishi sheria. Kama vile Mtume atakavyoonyesha katika Warumi 4, sheria ilitazamia injili inayokuja ya kuhesabiwa haki kwa imani, mbali na matendo ya sheria. Kwa hiyo, Injili huiweka sheria, ikitimiza utabiri wake yenyewe.
© 2024 The Enduring Word Bible Commentary by David Guzik – ewm@enduringword.com